24 Oktoba 2024 - 12:16
Syed Hashem Safiyyuddin, Mkuu wa Baraza Kuu la Hezbollah nchini Lebanon, aliuawa Shahidi

Hilo limetangazwa katika taarifa rasmi ya Hezbollah kwamba Syed Hashem Safiyyud_Din, Mkuu wa Halmashauri Kuu ya Hezbollah, ameuawa Shahidi katika njia ya kuelekea Quds (Jerusalem) baada ya shambulio la jinai la utawala haram wa Kizayuni.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul_Bayt (a.s) -ABNA-, Hezbollah ya Lebanon ilitangaza katika taarifa yake kwamba, Mkuu wa Halmashauri Kuu ya harakati hiyo, Syed Hashim Safiyyud_Din aliuawa Shahidi katika shambulio la utawala haram wa Kizayuni huko Beirut.

Kauli hii inasema: Kuuawa Shahidi Kiongozi Mkubwa na Shahidi Mkubwa katika njia ya kuelekea Quds, Mkuu wa Halmashauri Kuu ya Hezbollah Allamah Syed Hashim Safiyyud_Din (Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake), ambaye aliuwawa Shahidi akiwa sambamba na kundi la ndugu zake na Wapiganaji wake bora wa Jihadi katika shambulio la jinai ya Kizayuni.

Syed Hashim aliungana na Kaka yake aliyeuawa Kishahidi, Samahat al Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa Hezbollah, ambaye alikuwa ndugu na msaidizi bora kwa kaka yake, alikuwa kama Abul Fadhli al-Abbas (a.s) kwa kaka yake, Imam Hussain (a.s). Sayyid Hashim Safiyyudiyn alikuwa ndugu na mshika bendera, na aliaminiwa katika masaibu na matatizo, alikuwa Mcha_Mungu, Mtu Mwadilifu, Mshika Bendera, Muelekezaji na Mbunifu, Kiongozi na Shahidi.

Marhumu Shahidi Syed Hashem Safiyyudiyn alitumia maisha yake yote katika utumishi wa Hezbollah na Upinzani (Muqawamah) wa Kiislamu, na katika muda mrefu wa miaka mingi ya Umri wake mtukufu, akiwa na wajibu na mamlaka ya kushughulika na masuala ya Kiuongozi kwa Baraza Kuu na Taasisi mbalimbali na vitengo vya kiharakati katika nyanja zote na kila kitu kinachohusiana na Upinzani (Muqawamah) wa Hezbollah. Aliweza kuongoza mambo yote hayo kwa umri wake wote mpaka Mwenyezi Mungu alipomuunganisha katika msafara wenye nuru wa Mashahidi wa Karbala.